BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
BAADA ya kuisaidia timu yake ya Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, beki Abdi Banda ameweka wazi kuwa ataendelea kusalia kwa Wekundu hao msimu ujao.

Banda ambaye alifungiwa na timu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu dhidi ya Kocha Jackson Mayanja baada ya kugomea kuingia uwanjani katika mchezo dhidi ya Coastal Union, alisema hafikirii kwenda kokote hivyo bado ataendelea kuvaa jezi namba 24 ya Wekundu hao msimu ujao.

Banda ameiambia BOIPLUS kuwa katika maisha kuna mambo mengi yanatokea hasa kwa vijana lakini kwa sasa yamepita na wanasonga mbele kwa ajili ya Simba.

"Katika maisha vitu hivi vinatokea lakini hatuna budi kuviacha na kusonga mbele kwa ajili ya maendeleo ya Simba na mashabiki wake," alisema Banda.

Akizungumzia uhusiano wake na kocha Mayanja, Banda alisema hana tatizo lolote na Mganda huyo na wanafanya kazi pamoja na hakuna tofauti yeyote baina yao.

Banda ndiye mfungaji wa goli pekee la Simba dhidi ya Mtibwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na alionekana akishangilia kwa furaha pamoja kocha Mayanja kitu kilichoonesha kuzifuta tofauti zao.

Simba sasa wamefikisha alama 62 wakishika nafasi ya tatu wakisaliwa na mchezo mmoja dhidi ya JKT Ruvu Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top