BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
KIUNGO wa zamani wa Simba, Mohamed Banka amesema timu hiyo imepitia kipindi kigumu chenye machungu ya kukosa ubingwa kwa miaka minne sasa na kutamka kuwa ni wazi watakuwa wamejifunza kutokana na makosa.

Akizungumza na BOIPLUS, Banka alisema viongozi waache kuigiza na kutoa taarifa rahisi mbele ya jamii badala ya kukaa chini na kuweka mipango makini ambayo itawafanya Wanasimba, wawe na amani mtaani.

"Hii ni ajabu kama Rais wa Simba, Evance Aveva anathubutu kuahidi kusajili wachezaji wenye hadhi ambao wanatakiwa kutoa pesa ndefu wakati huo huo wanalalamika kukumbwa na ukata, hapo ndipo unaona siasa zinaendelea kutawala badala ya matendo ya kweli," alisema Banka.

Alisema kipindi ambacho Simba wamepitia ni cha machungu ambapo viongozi wangekuwa na nia basi wangekuwa wametengeneza timu iliyo bora na ushindani.

"Yaani miaka minne kukosa ubingwa Simba, ni aibu na ndiyo maana inapitia kwenye machungu haya, ndiyo maana hata utani wa maudhi kutoka kwa watani zao umeongezeka ila sasa siyo wakati wa kujibizana na watani wao bali waangalie walipojikwaa," alisema Banka.

Alisisitiza kwamba kuna haja ya kuwaita  wanachama kutoa michango yao na kudai kwamba kuna wanachama ambao wana pesa zao wanaweza kuichangia timu na ikarudi kwenye mstari.

Post a Comment

 
Top