BOIPLUS SPORTS BLOG

BIRMINGHAM, Uingereza
TIMU ya soka ya Aston Villa ambayo imeteremka daraja msimu huu katika ligi kuu ya Uingereza imenunuliwa na tajiri toka  ChinaTony Xia ambaye ni mfanyabiashara aliyewekeza katika sekta ya michezo, utalii, kilimo na afya.

Xia ambaye ameinunua Aston Villa kwa gharama ya dola 90 milioni, alisema amekuwa ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo kwa miaka mingi ingawa hajafurahishwa na matokeo mabovu ya msimu huu ambayo yamepelekea timu hiyo kushuka daraja.

Villa imeshuka daraja baada ya kuwa timu ya mwisho katika msimamo ikiwa na alama 17 tu.

Post a Comment

 
Top