BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
BEKI wa Yanga, Vincent Bossou raia wa Togo ametaja wachezaji 11 bora wanaocheza hapa nchini huku Amissi Tambwe yeye akikosekana kwenye kilosi chake hicho cha kwanza, badala yake akajumuishwa Hamis Kiiza wa Simba.

Bossou alikianika kikosi hicho kwenye ukurasa wake wa Facebook ambapo kiliongozwa na kipa Vincent Angban (Simba), Bossou, Pascal Wawa (Azam), Mbuyi Twite (Yanga) na David Assouman (Stand United).


Viungo ni Kipre Tchetche, Jean Mugiraneza wote wa Azam, Thaban Kamusoko na Haruna Niyonzima wa Yanga wakati washambuliaji ni Kiiza na Donald Ngoma (Yanga).

Katika kikosi hicho kinara wa mabao Tambwe raia wa Burundi hayupo pengine ataanzia benchi pamoja na wachezaji wengine wa kigeni ambao hajawataja kwenye kikosi chake cha kwanza.

Post a Comment

 
Top