BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Malimi Busungu ameshindwa kuendelea na mchezo timu yake ilipocheza na GD Sagrada Esperanca ya Angola baada ya kugongana na kipa wa timu hiyo Yuri Jose Tavazes ambapo aliumia kichwani sehemu ya utosini.

Busungu alitolewa kwa machela hadi nje ambapo alipewa huduma ya kwanza lakini baadaye walilazimika kumkimbiza hospitali ya Rufaa ya Taifa (Muhimbili) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kitu pekee ambacho kiliwatia hofu madaktari waliokuwepo uwanjani hapo ni damu iliyokuwa ikimtoka kichwani ambayo ilidhaniwa ikiachwa hivyo hivyo inaweza kuleta madhara makubwa.

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alilazimika pia kumuingiza Geofrey Mwashiuya kuchukuwa nafasi ya Busungu.

Katika mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam Yanga ilishinda bao 2-0 mabao ambayo yalifungwa na Simon Msuva pamoja na Matheo Anthony aliyetokea benchi akichukuwa nafasi ya Deus Kaseke.

Post a Comment

 
Top