BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Malimi Busungu atakosa mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya jana kuumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola ikiwemo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Azam na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne.

Katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda bao 2-0 ambapo mechi ya marudiano itachezwa Mei 18 nchini Angola, Yanga ikifuzu hatua hiyo itaingia hatua ya makundi.

Dakrati wa Yanga, Edward Bavu alisema kuwa Busungu alikimbizwa katika hospitali ya Temeke baada ya kulalamika maumivu kwenye mbavu huku akishonwa nyuzi nne utosini.

"Tulimpeleka hospitali ya Temeke kwa ajili ya uchunguzi kwani alikuwa akilalamikia maumivu ya mbavu, baada ya vipimo alilazwa ambapo ameruhusiwa asubuhi ya leo, ataendelea na matibabu ya siku saba, tutampa mapumziko ya siku saba zingine ndipo tutajuwa maendeleo yake zaidi hivyo inaweza kuchukuwa zaidi ya wiki mbili," alisema Dr Bavu.

Wakati huo huo, Yanga inatarajia kuondoka kesho Jumatatu asubuhi kwa kutumia usafiri wa anga kuelekea Mbeya kuikabili Mbeya City, mechi itakayochezwa keshokutwa Jumanne kwenye Uwanja wa Sokoine. Endapo Yanga itashinda mechi hiyo basi itatangaza rasmi ubingwa wao wa VPL.

Post a Comment

 
Top