BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, 
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kitakachoingia kambini Mei 23 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars utakaofanyika Nairobi Mei 29 na kumjumuisha Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa.

Stars itautumia mchezo huo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la mataifa barani Afrika dhidi  Misri mechi itakayopigwa Juni 4 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi kamili cha Stars ni kama ifuatavyo:

MAKIPA
Deogratius Munishi Dida' -Yanga
Aishi Manula - Azam
Benny Kakolanya - Prisons

WALINZI
Nadir Haroub - Yanga
Agrey Moris- Azam
David Mwantika - Azam
Haji Mwinyi - Yanga
Mohammed Hussein - Simba
Juma Abdul- Yanga
Andrew Vincent- Mtibwa
Erasto Nyoni- Azam

VIUNGO
Himid Mao - Azam
Mohammed Ibrahim - Mtibwa
Shiza Kichuya - Mtibwa
Jonas Mkude - Simba
Mwinyi Kazitomo - Simba
Ismail Issa Juma - JKU Zanzibar
Farid Musa - Azam
Juma Mahadhi - Coastal Union
Hassani Kabunda - Mwadui

WASHAMBULIAJI
Mbwana Samatta - KRC Genk
Thomas Ulimwengu - TP Mazembe
Ibrahim Ajib-  Simba
Elius Maguli - Stand United
Jeremia Juma - Prison
Deus Kaseke - Yanga

Post a Comment

 
Top