BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa
GWIJI wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa, Eric Cantona amemfananisha mshambuliaji Anthony Martial na Ronaldo de Lima.

Martial aliyejiunga na United kwa pauni 36 milioni akitokea Monaco majira ya kiangazi, ameonesha kiwango kikubwa kwa mashetani hao hasa goli lake la kwanza alilofunga dhidi ya Liverpool katika ushindi wa magoli 3-1.

Cantona alisema mshambuliaji huyo ni msumbufu kwa mabeki, anajua kuuchezea mpira, ana 'pua' ya goli kama ilivyokuwa kwa Mbrazil Ronaldo.

"Kwa umri wake, namtabiria kufika mbali yupo kwenye klabu kubwa inayothamini Wachezaji vijana, Angalia hata Cristiano Ronaldo alienda akiwa kijana lakini alitoka akiwa amekamilika kila Idara na kuwa miongoni mwa nyota tishio ulimwenguni," alisema Cantona.

Cantona pia alisema kujiunga kwa mshambuliaji huyo na United kutafungua mafanikio yake kwakuwa klabu hiyo ina mashabiki wengi ulimwenguni na imefanikiwa sana kibiashara.

Martial anatarajia kushuka dimbani leo katika uwanja wa Wembley katika fainali ya kombe la FA dhidi ya Cristal Palace huku akiwa kashaifungia timu yake magoli 17 na kusaidia upatikanaji wa magoli 11.

Post a Comment

 
Top