BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
KIUNGO mshambuliaji wa JKT Ruvu Hassani Dilunga amemaliza mkataba na maafande hao huku akiwa na asilimia chache za kuendelea kukikitumikia kikosi hicho msimu ujao.

Kiungo huyo ameiambia BOIPLUS kuwa kuna timu kadhaa zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake lakini hakuna waliofikia makubaliano yoyote kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao.

"Bado sijajua nitakuwa wapi msimu ujao lakini pia kuendelea kuwa hapa sidhani ila muda si mrefu nitajua mustakabali wangu," alisema Dilunga.

Dilunga pia alisema msimu unaoisha ulikuwa mgumu sana kwao na hawakutegemea kama wangesalia katika ligi hiyo kwakua ushindani ulikuwa mgumu huku wakiibuka katika michezo ya mwisho

Kiungo huyo aliyewahi kuitumikia Yanga na Mwadui alisema ilibidi uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wakae pamoja ili waone ni jinsi gani ya kuinusuru timu na janga la kushuka daraja.

Maafande hao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya 11 baada ya kukusanya alama 32 katika michezo yao.

Post a Comment

 
Top