BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
KWA mara ya kwanza katika historia ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), mwanamke, Bi Fatma Samba  Diouf ameteuliwa kuwa katibu mkuu mpya wa shirikisho hilo.

Bi Fatma ambaye ni raia wa Senegal anakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushika wadhifa huo wa juu katika shirikisho hilo na atasimamia shughuli za kila siku za shirikisho kwa muda wa mwaka mmoja.

Bi Fatma  ni mwanadiplomasia aliyehitimu ambaye kwa sasa amekuwa akihudumu kama mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa nchini Nigeria na amedumu kwa miaka 21.


Rais wa FIFA Gianna Infantino alimtangaza Bi Fatma kuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo katika kongamano kuu la FIFA linaloendelea nchini Mexico huku mwanamama huyo akikiri kuwa ni fahari kubwa kwake kupewa wadhifa huo.

Aliyekuwa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke alipigwa marufuku kujihusisha na shughuli zozote za soka kwa miaka 12 mapema mwaka huu baada ya kukutwa na tuhuma za Rushwa.

Post a Comment

 
Top