BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
STRAIKA mfaransa wa Arsenal, Olivier Giroud ameshtushwa na uvumi kuwa kocha Arsene Wenger amepanga kuleta washambuliaji wengine klabuni hapo hivyo anataka kuzungumza nae juu ya hatma yake.

Vyombo vya habari nchini Uingereza na Ufaransa vimekuwa vikiripoti kuwa baada ya kushindwa kunyakua ubingwa wa England kwa misimu mingi, Wenger ameamua kukijenga upya kikosi chake kiwe cha ushindani akiwa na mipango ya kuleta washambuliaji wa daraja la juu jambo ambalo limemtisha Giroud.

Giroud mwenye miaka 29, ameshindwa kung'ara klabuni hapo tangu aliposajiliwa mwaka 2012 na kwamba mabao 16 aliyofunga msimu huu pamoja na pasi kadhaa za mabao yameufanya huu kuwa ndio msimu wake bora zaidi tangu atue kwa washika bunduki hao.

Post a Comment

 
Top