BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu, Dar
WACHEZAJI wa kigeni wa Simba, wamegoma kwenda mjini Songea kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Majimaji itakayochezwa keshokutwa Jumatano.

Kikosi cha Simba kimeondoka leo asubuhi kwenda Songea kikiwa na wachezaji 13 pekee huku 'Maproo'  hao wakibaki jijini Dar es Salaam wakitaka kwanza walipwe mishahara yao ya mwezi uliopita.

Wachezaji hao ni Vincent Angban, Hamisi Kiiza, Emiry Nimubona, Justice Majabvi, Brian Majwega, Juuko Murshid na Raphael Kiongera ambaye anasumbuliwa na tumbo hivyo huyo aliondolewa mapema.

Simba inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58 imekwenda Songea ikiwa imetoka kupoteza mechi yake dhidi ya Mwadui iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa na kufungwa bao 1-0.

BOIPLUS inafahamu kwamba wachezaji wote wapo jijini Dar es Salaam wakiendelea na maisha yao kama kawaida.

Post a Comment

 
Top