BOIPLUS SPORTS BLOG

PRAGUE ,Czech
BINGWA mara sita wa michuano ya Olimpiki Usan Bolt ameweka rekodi mpya na bora zaidi katika  mbio za mita 100 nchini Jamhuri ya Czech.

Bolt alikimbia kwa chini ya sekunde 10 kwa mara ya kwanza, na kumaliza kwa sekunde 9.98 katika mashindano ya Golden Spike mjini Ostrava.

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukimbia Ulaya mwaka huu, na alijikwamua baada ya kuanza vibaya kwa kumshinda Ramon Gittens.

Bolt anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 na 200 na kabla ya mbio hizo Ostrava alisema atalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 200 mjini Rio mwezi Agosti.

Bolt alitumia sekunde 10.05 mbio zake pekee alizokimbia msimu huu, katika Cayman Islands Invitational huku mwanariadha huyo wa umri wa miaka 29 akipokea matibabu ya misuli ya paja baada ya mashindano hayo.

Bolt alichukua likizo baada ya mashindano ya ubingwa wa riadha duniani jijini Beijing Agosti mwaka jana ambapo alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 4x100m kupokezana vijiti.

Post a Comment

 
Top