BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Aliyekuwa Mwanza
KLABU ya Toto Africans ya jijini Mwanza imewafungia wanachama wake wanne kwa kuhusika na hujuma ikiwemo utovu wa nidhamu katika mechi yao iliyopita dhidi ya Yanga.

Wiki iliyopita, Toto ilikubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba matokeo ambayo yalisababisha mgogoro ndani ya klabu hiyo.

Wanachama waliofungiwa ni John Chief Kisura, Beatus Madenge na  Adamson Kibeta Ngassa ambao wanatuhumiwa kumpora fedha Katibu wa timu hiyo ambazo zinadaiwa kuwa zilikuwa za mgawo wa mapato ya mechi hiyo.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, Makamu Mwenyekiti,  Hamad Waziri Gao naye amesimamishwa kutokana na kuihujumu timu hiyo baada ya kutoa kauli kuwa Toto haiwezi kumfunga Yanga huku yeye akiwa kiongozi wake.

Baada ya mechi hiyo kumalizika viongozi wa Toto waligawanyika huku ikidaiwa baadhi yao walijiondoa kwenye maandalizi ya mechi hiyo ambapo pia wachezaji walituhumiana kuwa kuna baadhi yao wanahujumu timu kwa kucheza chini ya kiwango katika mechi hiyo.

Post a Comment

 
Top