BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
KOCHA Mkuu wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu 'Julio' amewaambia Simba kuwa wanatafunwa na laana ya kufukuza makocha wenye mapenzi ya dhati na timu hiyo na hicho ndicho kinacho kinachopelekea wafanye vibaya kwenue mechi zao.

Mbali na hilo Julio alisema kuwa baadhi ya viongozi wa Simba waliopo madarakani pia wanachangia kwa kiasi kikubwa timu yao kupata matokeo mabaya.

Julio alisema kuwa Simba iliwafukuza yeye na Abdallah Kibadeni licha ya kuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo na kufanya kazi kwa mapenzi kama nyumbani lakini haikuonekana thamani yao na sasa laana walioiacha inaendelea kuwatafuna.

"Kama sisi tulikuwa na matatizo au sio makocha wazuri mbona hadi leo Simba hawafanyi vizuri na tayari wametolewa kwenye Kombe la FA, hata mchezo wanaocheza ni wa kawaida sana kulinganisha na ukubwa wa timu,'' alisema Julio.

Julio na timu yake ya Mwadui imeingia jijini Dar es Salaam usiku wa jana wakitokea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuikabili Simba skeshokutwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa.

Mwadui wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kwa kukusanya alama 34 baada ya kushuka dimbani mara 26.

Post a Comment

 
Top