BOIPLUS SPORTS BLOG

Nitike Ahazi, Dar
KOCHA wa Majimaji ya Songea, Kali Ongala, amesema kuna haja kwa Shirikisho la Soka Tanzania  (TFF), kufungia viwanja ambavyo havina hadhi kwani vinaumiza wachezaji na  kushindwa kuonyesha uwezo wao.

Kali aliiambia BOIPLUS kuwa: "Wachezaji ni bora lakini viwanja siyo bora hii inawafanya wachezaji wawe kwenye mazingira magumu ya kufanya kazi pia inapelekea kukumbwa na adhabu za kadi kutokana na kucheza rafu zinazosababisha na ubovu wa viwanja hivyo,"

Kali alisema ubovu wa viwanja unasababisha kushindwa kupata wachezaji imara wa timu ya taifa kwani wanavyoandaliwa ni tofauti na mazingira wanayokwenda kuchezea.

"Mikoani kuna vipaji vikubwa kuliko hao ambao wanaonekana kwa urahisi wanaozichezea Simba, Yanga na Azam, ila wanapofika kucheza mechi jijini Dar es Salaam, hawawezi kucheza kwa ustadi.

"Wenzetu nje wanaendelea kwa sababu vitu muhimu vya kumuandaa mchezaji kama viwanja, gym, mipira, vinapewa kipaumbele. Naamini hata ikitokea mchezaji amesajiliwa kutoka nje ya nchi atashindwa kucheza kwa ajili ya viwanja," alisema

Post a Comment

 
Top