BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma
YANGA imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na jana Jumanne walidhihirisha kuwa wao ni wa kimataifa baada ya kuifunga Mbeya City bao 2-0 lakini kipa Juma Kaseja amekiri ubora wa Yanga kuwa walistahili kutwaa ubingwa huo.

Kaseja aliwapongeza Yanga na kuwataka wachezaji wengine kujituma na kutolewa sifa pale wanapofanikiwa kwani wanashindwa kutunza vipaji vyao pale tu wanapoanza kulewa sifa hizo.

Kaseja alisema Yanga walikuwa na ratiba ngumu lakini wameweza kutimiza malengo yao kwa kuhakikisha wanapigana kutetea ubingwa wao.

"Walistahili kuchukua ubingwa wana wachezaji wazuri kikosi chao kipana kwahiyo nawapa hongera zao sisi tutaangalia msimu ujao," alisema  Kaseja

Kaseja alijiunga na Mbeya city msimu huu akitokea Yanga kwa mkataba wa miezi sita ambao unamalizika mwezi Juni na aligoma kuweka wazi mipango yake.

Post a Comment

 
Top