BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
LICHA ya kupata mapokezi makubwa kwa klabu yake beki mpya wa Yanga, Hassani Kessy amekiri itakuwa ngumu kupata namba kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa Simba.

Kessy ambaye anacheza nafasi ya beki wa kulia itabidi achuane vikali na Juma Abdul ambaye yupo katika kiwango bora na amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa tano pamoja michuano ya kombe la FA.

Kessy ambaye alitambulishwa kwa wapenzi na wanachama wa timu hiyo katika mechi ya fainali ya kombe la FA jana aliiambia BOIPLUS kuwa anamuheshimu sana Juma na atajifunza vitu vingi kutoka kwake ili kuendelea kuwa katika kiwango bora.


"Kwanza namkubali sana Juma, yupo katika ubora mkubwa na kucheza pamoja nae itaniongezea kujiamini na kujituma zaidi," alisema Kessy.

Kessy pia alisema alisaini kwa mabingwa hao wa kihistoria huku akijua ataenda kucheza kwa kupokezana ili kuongeza changamoto ya kujituma zaidi na kuwa bora.

"Ili ufanikiwe lazima ujifunze kwa waliofanikiwa, kupitia Yanga nitaweza kucheza soka la kimataifa japokuwa nitacheza kwa kupokezana na Juma," alimalizia Kessy.

Yanga walimsajili beki huyo aliyetoka kwa watani wao wa jadi Simba kabla ligi haijamalizika  baada ya kukwaruzana na uongozi wa Wekundu hao.

Post a Comment

 
Top