BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Sheila Ally, Dar
KIUNGO wa Mtibwa Sugar, Shiza Kichuya huenda msimu ujao akavaa uzi mwekundu baada ya kuelezwa kwamba juzi Alhamisi alisaini mkataba wa awali wa miaka miwili na Simba.

Usajili wa mchezaji huyo umefanywa kwa kificho kikubwa kwani Kichuya ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar ingawa kuna taarifa kwamba vigogo hao wana mpango wa kwenda kumalizana na bosi wa Mtibwa.

Simba walianza kumtolea macho Kichuya tangu msimu huu kutokana na uwezo wake alioonyesha ambapo aliwahi kuteuliwa mwa mchezaji bora wa mwezi katika ligi iliyomalizika.

"Kilichobaki ni kwenda kumalizana na viongozi wake, ni mchezaji mzuri labda suala la mkataba lizingue kwenye malipo," alisema kiongozi huyo.

Simba imetajwa pia kumbana Hassan Kabunda wa Mwadui ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo na tayari viongozi wa Mwadui wamefungua milango ya mazungumzo na Simba japokuwa Wekundu hao bado hawajaanza safari ya kwenda Shinyanga pamoja na Idd Mobi ambaye mkataba wake umemalizika.

Wakati huo huo, kocha Jackson Mayanja juzi aliondoka kurudi kwao Uganda ikiwa ni siku chache tangu akabidhi taarifa yake ya utendaji kwa viongozi wake ambayo imeelezwa kutaja wachezaji watakaotemwa na wale watakaoachwa pamoja na mapendekezo ya majina ya wachezaji wapya watakaosajiliwa.

Post a Comment

 
Top