BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF limetangaza viingilio vya mechi ya Fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Azam na Yanga utakaofanyika Kesho katika uwanja wa Taifa jijijini Dar es Salaam.

Sherehe za mchezo huo zitaanza rasmi saa 8.00 mchana kwa mchezo wa awali wa kuburudisha utakaokuzikutanisha timu za soka za kituo cha Televisheni cha Azam ‘Azam Tv’ na wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kurushwa live na kituo hicho.

Viingilio katika mchezo huo itakuwa ni Sh 25,000 kwa VIP A wakati VIP B na C ni Sh 20,000 wakati majukwaa yenye viti vya rangi ya chungwa, mzunguko wenye viti vya rangi ya bluu na kijani ni Sh 5,000.

Kwa mujibu wa kanuni bingwa wa michuano hiyo atatwaa kombe, medali na fedha Sh 50 milioni wakati mshindi wa pili atazawadiwa tuzo na medali. Kadhalika kutakuwa na tuzo kwa mchezaji bora, mfungaji bora na mchezaji bora wa michuano hiyo ambayo waaandaaji wamepanga kuiboresha mwakani.

Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam  huku akisaidiwa na Ferdinand Chancha wa Mwanza upande wa kulia (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia. Kamishna wa mchezo huo anatakuwa Juma Mgunda wa Tanga.

Post a Comment

 
Top