BOIPLUS SPORTS BLOG

MUNICH, Ujerumani
ATLETICO Madrid imetinga hatua ya fainali ya ligi mabingwa barani ulaya licha ya kufungwa magoli 2-1 na Bayern Munich katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich.

Bayern ambao walianza mchezo huo kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi walipata goli la kwanza dakika ya 31 kupitia kwa Xabi Alonso kwa mpira wa adhabu ndogo nje ya eneo la 18.

Dakika mbili baadae beki Jose Maria Gimenez alimfanyia madhambi Lewandowsky na kusababisha penati ambayo ilipigwa na Thomas Mueller, mlinda mlango wa Atletico Oblack alipangua.


Antoiny Griezmann ndiye aliyeipatia Atletico Madrid goli la kusawazisha baada ya kupokea pasi ya Fernando Torres kabla ya Robert Lewandowsky kuwafungia wenyeji goli la pili dakika ya 74.

Fernando Torres nae alikosa penati dakika ya 84 baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari na Javier Martinez na golikipa Manuel Nuer kucheza mkwaju huo.

Atletico wanasubiri mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City wacheze fainali katika uwanja wa Guissepe Meazza Mei 28.

Post a Comment

 
Top