BOIPLUS SPORTS BLOG

MEI 18 katika uwanja wa St Jakob-Park, Basel huko nchini Uswisi kutapigwa kipute cha fainali ya ligi ya EUROPA ambapo mabingwa watetezi Sevilla ya Spain watakutana na majogoo ya Anfield, Liverpool.

Sevilla wametinga fainali kwa kuifunga Shakhtar Donetsk mabao 3-1 katika uwanja wa  Estadio Ramon Sanchez Pizjuan Jijini Sevilla, Hispania.

Katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa wiki iliyopita huko Ukraine, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 hivyo mabao ya Kevin Gameiro (2) na Mariano Ferreira 'Filho' yaliifanya Sevilla yatinge fainali kwa jumla ya mabao 5-3.

Liverpool ambao waliambulia kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa awali dhidi ya Villareal wiki iliyopita, jana walifanikiwa kuwageuzia kibao wahispaniola hao na kuwatandika mabao 3-0 kwenye uwanja wa Anfield.

Shukrani za pekee ziwaendee Daniel Sturridge na Adam Lallana walioifungia Liverpool huku bao jingine likifungwa na Bruno Soriano wa Villareal aliyejifunga katika harakati za kuokoa mpira huku wahispaniola hao wakilazimika kucheza pungufu kwa dakika 20 kufuatia Victor Ruiz kupewa kadi ya nyekundu katika dakika ya 70.

Post a Comment

 
Top