BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
WASHAMBULIAJI wa Simba, Danny Lyanga na Hijja Ugando wanasubiri vipimo zaidi ili kubaini tatizo lao baada ya kuumizwa katika mchezo yao dhidi ya Azam iliyichezwa jana Jumapili na kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa machela.

Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare tasa huku Daktari wa timu hiyo  Yassin Gembe akiitonya BOIPLUS kuwa  ni mapema mno kutoa jibu moja kwa moja juu ya maumivu yao ila majibu hayo yatatolewa baada ya vipimo vinavyotarajiwa kufanyika kesho.

"Kwa sasa wote wanaendelea vizuri lakini tutawafanyia vipimo zaidi kesho ili kujua wameumia kwa kiasi gani na tutatoa majibu ya vipimo hivyo," alisema Gembe.

Endapo vipimo hivyo vitaonyesha kuwa wachezaji hao wameumia sana basi litakuwa pigo kubwa kwa Simba ambayo imebakiza mechi nne za Ligi Kuu Bara na kucheza mechi 26 zilizowapa pointi 58 na kuituliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Simba imepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa baada ya kupoteza mechi hiyo ambapo ipo nyuma kwa pointi daba dhidi ya Yanga wanaoongoza kwa pointi 65 nao wamebakiza mechi nne.

Post a Comment

 
Top