BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
MSIMU mpya wa shindano la Maisha Plus utakao shirikisha washiriki kutoka nchi tano za Afrika Mashariki umezinduliwa katika viwanja vya Uhai Production vilivyopo Tabata jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo litakuwa na washiriki 30 huku 16 wakitoka nje ya nchi 14 pekee ndiyo wazawa ambao watapeperusha bendera ya Tanzania.

Mkurugenzi mtendaji wa Maisha Plus, Masoud Kipanya alisema msimu huu ambao utaanza kuoneshwa kupitia king'amuzi cha Azam TV kuanzia Jumapili ya Mei 29 vipindi vyake vitakuwa na muonekano bora kulinganisha misimu iliyopita huku mshindi akiibuka na Sh 30 milioni.


Naye Mkurugenzi mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alisema Maisha Plus ni kipindi kinachoonesha maisha halisi ya kijana wa kiafrika na kimekuwa msaada mkubwa kwa ajili ya kubadilisha mitazamo kwa watu wengi ambao walikata tamaa.

Huo unakuwa ni msimu wa tano shindano hilo ambalo linazidi kuteka hisia za watazamaji wengi kutokana na washiriki wake kuishi maisha ya asili.

Post a Comment

 
Top