BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Mwandishi Wetu
WINGA wa Simba, Brian Majwega ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuelezea hisia zake juu ya kocha wa timu hiyo, Jackson Mayanja 'Mia mia' ambaye ni raia mwenzake wa Uganda.

Majwega ambaye hakupata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, amefunguka kuwa hatokuja kumsamehe Mayanja kwa aliyomfanyia na anamshukuru kwa kummaliza kimpira ikiwa ni pamoja na kusambaza maneno ya uongo juu yake.

"Sijui familia yangu ilimkosea nini Mayanja, ila maisha yanaendelea,  namshukuru kwa kunionyesha jinsi ya kukabiliana na mambo kama haya. Namtakia kila la heri katika maisha yake lakini kamwe sitokuja kuwa pamoja na watu wa aina hii," alieleza Majwega katika andiko hilo

Mayanja amedaiwa kuwa katika mahusiano mabaya na wachezaji wanaotoka Uganda ambao ni Majwega, Hamis Kiiza na Juuko Murshid na tayari aliwahi kutofautiana na Kiiza.

Post a Comment

 
Top