BOIPLUS SPORTS BLOG

✏Bakari Kagoma, Dar
Mwili wa marehemu Said Pamba ukiombewa kabla ya kupelekwa makaburini

MAZISHI ya aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba awamu iliyopita, Saidi Pamba yamefanyika katika makaburi ya Mnazi mmoja Manzese leo Saa saba mchana huku mamia ya wapenda michezo wakihudhuria.

Pamba alifariki dunia ghafla jana katika hospitali ya Mbezi ambako alipelekwa juzi baada ya kuugua maradhi ya shinikizo la damu na kisukari.

Rais Aveva akizungumza na baadhi ya mashabiki wa Simba ambao walitumia nafasi hiyo kumshauri juu ya kuijenga timu yao

Miongoni mwa waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa klabu hiyo Evans Aveva aliyeambatana na makamu wake Godfrey Kaburu, Haji Manara, Hassan Dalali, wajumbe Ally Suru, Said Tully, Sweddy Mkwabi ambaye alifanya kazi na Pamba ndani ya Simba, pamoja na mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro.

Manara akizungumza na Muro msibani hapo

Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Simba waliohudhuria mazishi hayo walimwelezea Pamba kama mchapakazi na mwenye ushauri bora huku akisifiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuishi vizuri na wachezaji.

"Huyu jamaa alikuwa anajua jinsi ya kuishi na wachezaji, hata kama mshahara haujatoka au wana madai flani, Pamba akiongeanao walikuwa wanatulia na kucheza mpira kama hakuna tatizo lolote," alisema Mkwabi.


Pamba ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama cha soka wilaya ya Kinondoni (KIFA) ameacha mke na watoto watatu.


Post a Comment

 
Top