BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
LEICESTER City leo ilikuwa inahitaji ushindi dhidi ya Manchester United ili itangaze Ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, ila sasa unajua walichofanya mashetani hao wekundu?, ni kuibania kwa sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

United walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya nane liliwekwa nyavuni na kinda Antony Martial kufunga akiunganisha krosi ya mlinzi Antonio Valenciai

Leicester walisawazisha bao hilo katika dakika ya 17 kupitia kwa nahodha Wes Morgan aliyeuparaza kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo Danny Drinkwater.

Leceister ilipata pigo katika dakika ya 86 baada ya Drinkwater kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumwangusha Memphis Depay kwa makusudi hivyo kuwafanya mabingwa hao watarajiwa wacheze wakiwa pungufu kwa takribani dakika saba.

Post a Comment

 
Top