BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma
MANCHESTER United imenyakua taji la ubingwa wa kombe la FA baada ya kuifunga Cristal Palace 2-1 katika uwanja wa Wembley jijini London katika muda wa nyongeza.

Mashetani wekundu walionekana kucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini ni Palace ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 78 kupitia kwa Jason Puncheon kabla Juan Mata hajasawazisha dakika ya 81.


Mechi ilienda muda wa nyongeza baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya goli 1-1.

Dakika ya 105 beki Chris Smalling alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Bolasie na kuwafanya United kucheza pungufu kwa dakika 15 za mwisho.


Jesse Lingard ndiye alikuwa shujaa wa United baada ya kuifungia goli la ushindi dakika ya 110 kufuatia mabeki wa Palace kushindwa kuokoa hatari langoni kwao.

Mara ya mwisho kwa United kuchukua ubingwa huo ilikuwa mwaka 2014 baada ya kuifunga Milwall magoli 3-0, hii ni mara ya 12 kwa mashetani hao kunyakua taji hilo.

Post a Comment

 
Top