BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
KIPA wa Azam, Aishi Manula ndiye alidaka mechi nyingi za Ligi Kuu ndani ya kikosi hicho ambapo amefichua siri ya mafanikio yake kwamba anapata muda wa kujifunza kutoka kwa makipa wenzake wawapo mazoezini.

Manula aliiambia BOIPLUS kuwa: "Sijibweteki na kujiona nimemaliza kila kitu bali napenda kujifunza mbinu kutoka kwa wenzangu naamini wana viwango vizuri ila tunatofautiana nyakati za kufanya kazi," alisema.

Manula alisema anajua ana ushindani mkali mbele ya Ivo Mapunda na Mwadini Ally ambao anaamini kwamba wana uwezo na ndiyo chachu ya yeye kufanya vizuri.

"Mapunda na Mwadini wasingekuwa na kiwango kizuri basi nisingekuwa kwenye uwezo 
huu kwa sababu najua nikifanya vibaya benchi linakuwa linanisubiri, hivyo 
napambana kadri niwezavyo," alisema Manula.

Post a Comment

 
Top