BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
KIKUNDI cha mashabiki wa timu ya Simba ' Simba Sports Club Upendo' kimemchagua beki wa kushoto wa timu hiyo Mohamed Hussein 'Tshabalala' kuwa mchezaji bora wa msimu.

Kiongozi wa kikiundi hicho Mbaraka Shomari alisema japokuwa timu yao haikufanya vizuri msimu huu lakini Tshabalala alikuwa katika kiwango bora na kuwafanya kumchagua mchezaji bora wa msimu.

Tshabalala alipata zawadi ya jozi ya viatu vya kuchezea mpira yenye thamani ya sh 90,000 kwa ajili ya kumhamasisha kuendelea kujituma zaidi na msimu ujao aendelee kuwatumikia Wekundu hao.

"Hatuna kikubwa cha kukupa kwa kuonesha mchango wako kwenye klabu yetu tulichokipata ndiyo hicho tunakuomba upokee japokuwa kuna Wachezaji wengine walifanya vizuri sana ila kwetu wewe ndiyo mchezaji bora wa msimu" alisema Shomari akikabidhi zawadi hiyo.

Kwa upande wake beki huyo aliwashukuru wadau hao kwa kuthamini mchango wake ndani ya Simba na kuwaahidi ataendelea kupambana ili kuwapa raha mashabiki na wanachama wa klabu hii.

"Nachukulia zawadi hii kama changamoto kwangu kuendelea kujituma ili nisiwaangushe wapenzi wangu ambao mmeonesha kuthamini mchango wangu ndani ya Simba," alisema Tshabalala.

Tshabalala alisajiliwa na Simba akitokea Kagera Sugar msimu wa 2014/15 na sasa amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo ndani ya timu.

Post a Comment

 
Top