BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
LICHA ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu Kocha wa Simba, Jackson Mayanja ametamka wazi kuwa yeye ni kocha bora anayestahili kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Mayanja alisema tangu aanze kuifundisha Simba katika michezo 20 ya ligi ameshinda mechi 17, amepoteza michezo mitatu pekee huku akisema takwimu hizo zinaonyesha ni jinsi gani habahatishi katika kazi yake.

"Niliikuta timu katika mazingira magumu tulipambana na kuifikisha timu hapo ilipo kuna vitu vidogo tu  kurekebisha tuwe na kikosi bora msimu ujao," alisema Mayanja.

Kauli hiyo imeungwa mkono na kocha wa JKT Ruvu,  Abdallah Kibadeni na kusema Simba itafanya makosa endapo itamfuta kazi Mganda huyo kwakuwa amefanya mageuzi makubwa ndani ya kikosi na endapo atapewa muda zaidi atafanya makubwa zaidi msimu ujao.

"Mayanja ni kocha mzuri itakuwa sio busara kwa uongozi wa Simba kumfukuza kwakuwa ameshaanza kujenga kikosi imara," alisema Kibadeni

Mayanja alirithi mikoba ya kocha Muingereza Dylan Kerr mwanzoni mwa mwaka huu na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya tatu.

Post a Comment

 
Top