BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
FAINALI ya kombe la FA kati ya Yanga na Azam ambayo ilikuwa ichezwe Juni 11, sasa itapigwa Mei 25 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam saa 10 jioni.

Akizungumza kuhusu mabadiliko ya ratiba hiyo Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Alfred Lucas alisema wameirudisha nyuma fainali hiyo ili  kupisha maandalizi ya timu ya Taifa itakayocheza na Misri Juni 4.

Lukas alisema kutokana na umuhimu wa mechi dhidi ya Misri wamerudisha nyuma fainali hiyo kumpa nafasi kocha wa Stars kuandaa timu japo kwa wiki moja kuhakikisha wanapata alama tatu toka kwa Mapharao.

Stars itaingia kambini Mei 23 baada ya kumalizika kwa ligi na siku mbili baadae itafanyika fainali hiyo kisha kuelekea jijini Nairobi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya Mei 29.

Wadau mbali mbali wa soka nchini wamekuwa wakichukizwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba yanayofanywa na shirikisho hilo.

Post a Comment

 
Top