BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
MECHI ya Yanga na Ndanda FC iliyopangwa kuchezwa Mei 15 sasa imerudishwa nyuma na itachezwa Mei 14, mechi hiyo itapigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mabadiliko hayo ya ratiba yamefanyika leo ya Jumatatu na Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kutaja sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 ni kuipa nafasi Yanga ya kujiandaa na safiri ya kwenda Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8 badala ya Mei 7, 2016.

Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Yanga dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.

Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8,  badala ya Mei 7, sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga utakuwa na mchezo kati ya Stand United dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Kadhalika hiyo, inatarajiwa kuendelea  kesho Jumanne kwa mchezo mmoja ambao Yanga ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Jumatano Mei 4, Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, mechi itakayocheza Uwanja wa Chamazi.

Post a Comment

 
Top