BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Bakari Kagoma, Dar
WANACHAMA, wapenzi na mashabiki wa Simba wametakiwa kutulia na kuendelea kuonesha umoja wao katika kipindi hiki kigumu ambacho klabu yao inapitia.

Nahodha wa timu hiyo Musa Hassani Mgosi aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa pambano la ligi kuu dhidi ya Azam hapo jana ambapo aliwaasa wanamsimbazi kuwa sasa sio muda wa kulumbana na  kumtafuta mchawi badala yake wasubiri hadi mwisho wa ligi ambapo itafahamika wapo nafasi gani na hapo ndipo wataanzia kuelekea msimu ujao.

"Tukiendelea kulumbana ndiyo tutapotea zaidi ya hapa kikubwa ni kuvuta subira ligi iishe ndiyo tushikane mashati, kama ni sisi wachezaji, benchi la ufundi au viongozi, kama kuna aliyehusika katika hili basi awajibishwe," alisema Mgosi.

Akizungumzia mustakabali wake ndani ya Simba Mgosi alisema kama watapenda kuendelea nae msimu ujao yeye yuko radhi na wakiona hana nafasi basi atatafuta mahali kwingine kwavile mpira ndiyo kazi yake na hana mpango wa kustaafu miaka ya hivi karibuni.

Mkataba wa Mgosi na Simba unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu huku nahodha huyo pia akitumika kama kocha mchezaji.

Post a Comment

 
Top