BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
Marehemu Said Pamba (kulia) akiwa na Zacharia Hans Poppe kwenye moja ya vikao enzi za uhai wake

ALIYEKUWA mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage, Saidi Pamba amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospital ya Mbezi jijini Dar es Salaam.

Saidi alikuwa akisumbuliwa na Kisukari pamoja na Shinikizo la damu kwa muda mrefu alishinda vizuri jana akiwa na afya nzuri kabla hali yake haibadilika na kukimbizwa hospitali ya Mbezi usiku na asubuhi aliaga dunia.

Aliyekuwa mjumbe mwenzake katika klabu ya Simba Sweddy Mkwabi alisema msiba upo nyumbani kwa Dada wa marehemu Manzese Darajani  ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho saa 5 asubuhi.

" Tumepoteza mtu muhimu katika medani ya mpira nchini, alikuwa mtu anayesikiliza ushauri na mwenye msimamo katika mambo yake, Siku zote vizuri huwa havidumu," alisema Mkwabi kwa majonzi mazito.

Marehemu pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji wa chama cha soka Manispaa ya Kinondoni KIFA hadi anafikwa na umauti.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu.
INNA LILAH WAINNAH ILAHIL RAJIUN.

Post a Comment

 
Top