BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
KOCHA Mkuu wa timu ya soka Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Mei 18 anatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji  wakaokwenda Kenya kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Mei 29

Taifa Stars, itatumia mchezo huo utakaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa ajili ya kujiandaa dhidi ya  Misri katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON). 

 Stars itamenyana na Misri June 4 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top