BOIPLUS SPORTS BLOG

✏MANCHESTER, Uingereza
KOCHA mahiri Jose Mourinho leo ametangazwa rasmi kuwa meneja wa Manchester United ya Uingereza kuanzia msimu wa 2016/17 huku mashetani hao wakiweka kipengele maalumu cha kumpa mreno huyo nafasi ya kuendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.

Mourinho mwenye tabia ya kuhama timu mara kwa mara, amepewa mkataba wa miaka mitatu lakini unaompa nafasi ya kuendelea kuwepo hapo hadi angalau 2020.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 amefanikiwa kubeba makombe 22 tangu mwaka 2003 huku uzoefu wake ndani ya ligi kuu ya Uingereza ukiwapa kiburi United kuwa kocha huyo atafanikiwa katika timu yao.

Post a Comment

 
Top