BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba Madelu kesho  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda na Young Africans utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya Nchemba ambaye atakabidhi Kombe kwa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi hiyo msimu wa 2015/16, wageni wengi maalumu watakaokuwa kwenye mchezo huo ni Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi ya Kuu Tanzania Bara (TBLB).

Mchezo huo utafanyika kwa baraka za TPLB baada ya maombi ya Yanga kukubaliwa na Ndanda ambao watakuwa wenyeji wa mchezo
huo utakaoanza saa 10:00 alasiri.

Mara baada ya mchezo huo, Mabingwa watapewa Kombe la ubingwa, medali na fedha Sh 81,345,723; Mshindi wa Pili Sh
40,672,861; Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 na Mshindi wa Nne atazawadiwa Sh 23,241,635. Mchezaji Bora atapewa Sh 5,742,940 sawa na Mfungaji Bora wa Ligi na Kipa bora wa michuano
hiyo inayodhaminiwa na Vodacom, Bia ya Kilimanjaro, Azam, Startimes na NHIF. Mwamuzi Bora atazawadiwa Sh 8,614,610 saw na 

Kocha Bora wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh
17,228,820. Yanga ndiyo iliyoomba kwa Ndanda
kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo
kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri kwa ndege Jumapili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada
Esperanca ya Angola utakaofanyika ama Mei 17
au 18, mwaka huu.

Barua ya Bodi ya Ligi kwa  imesema kwamba Yanga watatumia mchezo huo ambao Ndanda itakuwa mwenyeji kupokea taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litakalotolewa na Nchemba ambaye mara nyingi anaonekna uwanjani.

Kanuni ya pili ya Ligi Kuu Bara toleo la 2015/16 imeeleza wazi kuwa, “Katika mazingira maalumu, timu inaweza kucheza mchezo wake wa nyumbani katika uwanja mwingine endapo kuna sababu nzito na za msingi, utambulisho wa uwanja katika
mazingira haya pia unawajibika kufanywa katika
kipindi cha uthibitisho wa kushiriki ligi au kwa maombi maalumu kwa TPLB,” inasehemu kanuni hiyo. Kwa kuzingatia kanuni hiyo na sababu za yanga ambazo Ndanda na Bodi wameona kuwa ni nzito wamekubaliana kucheza mchezo huo Dar es Salaam.

Tayari Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi ameipongeza timu ya soka ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita wa mwaka 2014/2015.

Hii ni mara ya 26 kwa Yanga ambayo kwa sasa inacheza mashindano ya kuwania kutwaa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kutwaa taji hilo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara
mwaka 1965. Simba inafuatia katika rekodi hiyo baada ya kulitwaa taji hilo kwa mara 18.

“Nichukue nafasi hii Kuipongeza Yanga
kwa ubingwa. Pia nizipongeze timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya
msimu wa Ligi Kuu Bara ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio,” amesema Rais Malinzi

baada ya Yanga kufikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine 15 zilizoshiriki ligi hiyo.

Post a Comment

 
Top