BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza
Jose Mourinho ameteuliwa kuwa kocha mpya  Manchester United kuchukua nafasi ya Luis Van Gaal aliyetimuliwa mapema wiki hii.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 53 amesaini mkataba na Mashetani hao katika hotel ya Central London jioni ya leo huku akiwa na furaha baada ya kutimiza ndoto zake.

Wakala wake Joge Mendez alikutana na Mkurugenzi mtendaji wa United Ed Woodward mapema wiki hii kwa ajili ya kumalizia dili hilo.

Mourinho amehitimisha miezi sita ya kukaa bila kazi baada ya kutimuliwa Chelsea mwezi Disemba mwaka jana.

Taarifa zinasema Mreno huyo alikuwa apewe kibarua hicho mara baada ya Mdachi Luis Van Gaal kuanza kuvurunda.

Post a Comment

 
Top