BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
NYOTA wa Yanga, Haruna Niyonzima na Geofrey Mwashiuya wameteka akili ya msanii maarufu wa Bongo Movie aliyewahi pia kuwa Miss Tanzania 2007, Wema Sepetu ambaye ametamka kuifuata Yanga jijini Mbeya kwa ajili ya kuishangilia ikicheza na Mbeya City.

Wema alikuwepo uwanjani jana akishuhudia Yanga ikipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya GD Sagrada Esperanca ya Angola, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Yanga itacheza na Mbeya City keshokutwa Jumanne, Uwanja wa Sokoine.

Katika mechi hiyo Niyonzima na Mwashiuya walionekana kupambana kuhakikisha timu yao inatwaa ushindi huo ambapo Mwashiuya alisababisha bao la kwanza kwa kumpigia krosi safi kwa  Simon Msuva.


Wema alisema kuwa huwa anapata faraja pale Yanga inapofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mashindano ya ndani ambayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

"Mechi zozote ambazo Yanga wancheza huwa nafurahi sana hasa pale wanaposhinda. Nitaenda kuishangilia popote itakapokwenda iwe ndani ya nchi ama nje ya nchi, kiukweli  Niyonzima na Mwashiuya wanajua soka na ni wapambanaji kuhakikisha ushindi unapatikana na hilo ndilo linalotakiwa,'' alisema Wema.

Wema alisema miaka iliyopita alisusa kwenda uwanjani baada ya timu yake kufungwa na Simba mara kwa mara kwani alikuwa anaumizwa sana na matokeo hayo mabaya yaliyokuwa yanachangia ashindwe kufanya majukumu yake ipasavyo.

''Najiandaa kwenda Mbeya ila kiukweli  msimu uliopita nilikuwa navutiwa sana na Amissi Tambwe jinsi alivyokuwa anapambana uwanjani, Yanga ni timu bora,'' alimaliza Wema.

Post a Comment

 
Top