BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
MWAMUZI mkongwe nchini, Israel Mujuni Nkongo wa jijini Dar es Salaam,  ndiye atakayechezesha mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Azam itakayochezwa keshokutwa Jumatano, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utaanza saa 10.30 jioni huku waamuzi wasaidizi wakiwa Ferdinand Chacha wa Mwanza,  Soud Lila wa Dar es Salaam na mwamuzi wa mezani ni Frank Komba wa Dar es Salaam huku Kamishna wa mchezo huo ni Juma Mgunda wa Tanga.

Fainali za Kombe la Shirikisho zinakuja baada ya mchuano ulioshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24)

Post a Comment

 
Top