BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
BEKI wa kulia wa timu ya Yanga, Juma Abdul amechagulia kuwa mchezaji bora wa michuano ya kombe la FA baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika mashindano hayo.

Abdul Pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya fainali baada ya kuonyesha uwezo mkubwa huku akisaidia kupatikana kwa goli la kwanza lililofungwa na Amisi Tambwe.

Beki huyo amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ya Yanga pia akichangia upatikanaji wa mabao mengi huku pia yeye mwenyewe akifunga katika mechi kadhaa kwa mtindo wa mashuti makali. 

Atupele Green wa Ndanda FC ameibuka mfungaji bora wa michuano baada ya kufunga magoli matano na kuwazidi washambuliaji wengine ambao walishindwa kufikia idadi hiyo.

Aishi Manula wa Azam ndiye golikipa bora wa michuano hiyo ambayo imechezwa msimu huu baada ya miaka 14 kupita.

Post a Comment

 
Top