BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Morogoro
 Simba iliifunga Mtibwa bao 1-0 jana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Pichani ni mfungaji wa bao hilo pekee, Abdi Banda

 Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala' akijiandaa kupiga krosi.

 Kama mnamchukulia poa Mussa Hassan 'Mgosi' kwavile mara nyingi anakaa benchi basi kwa Mtibwa huyo ni mtu hatari sana. Mgosi ndiye mshambuliaji aliyeisumbua zaidi ngome ya Mtibwa jana, hapa anaonekana akichungwa na wachezaji wanne wa Mtibwa

 Mgosi akiwatoka walinzi wa Mtibwa, Andrew Vicent (kushoto) na Issa Rashid 'Baba Ubaya'

 Ally Sharif wa Mtibwa akijiandaa kumzuia Said Ndemla asikatize na mpira huku nahodha Shaban Nditi akisubiri kutoa msaada

 Vicent akiokoa mpira katikati ya mstari wa goli. Mpira huo uliokuwa ukielekea langoni huku Said Mohamed akiwa ameshapotea, almanusura uipatie Simba bao katika kipindi cha kwanza

 Kipa wa Simba aliyekuwa benchi jana, Vicent Angban akimbeba Banda baada ya kuifungia bao timu hiyo. Kushoto ni walinzi Novaty Lufungo na Mohamed Fakih

 Hussein Javu akimkwatua Tshabalala aliyekuwa anaingia eneo la hatari la Mtibwa

 Baba Ubaya akimchunga kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto

 Kipa Mohamed akiwa ameduwaa huku mpira ukijaa wavuni.

 Kipa wa Mtibwa, Hussein Sharif 'Cassilas' akiwa jukwaani wakati pambano hilo linaendelea

Beki wa zamani wa Simba ambaye amesaini kuichezea Yanga, Hassan Kessy (mwenye kofia) akiwa jukwaani kushuhudia mchezo kati ya Mtibwa na Simba

Post a Comment

 
Top