BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi, Dar

Huu ni msafara wa kikosi cha Yanga iliyorejea kutoka nchini Angola ambako ilifanikiwa kutinga hatua makundi ya kombe la shirikisho

 Kocha wa Yanga, Hans Pluijm na msaidizi wake Juma Mwambusi mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere

 Wachezaji na viongozi wa Yanga wakitoka nje na kulakiwa nanmamia ya mashabiki waliofurika uwanjani hapo

 Shujaa wa Yanga, kipa Deogratius Munishi 'Dida' akiwa ameshika mfano wa mdege yenye neno WAKIMATAIFAThaban Kamusoko na Donald Ngoma wakipakia mizigo yao kwenye toroli ili kwenda kupanda basi lililowapeleka kambini

 Shabiki huyu aliyevalia kama mganga wa jadi alikuwa kivutio uwanjani hapo.

 Ukifika uwanja wa Taifa ukiwa umevaa nguo yenye rangi nyekundu usithubutu kukatisha kwenye jukwaa lenye mashabiki wa Yanga. Hali ilikuwa ni tofauti kabisa na leo ambapo hakuna rangi ilikosekana katika msafara huoHuyu naye alitaka kutumia fursa ya wingi wa watu kufanya uporaji wa simu. Kilichomkuta ndio hiki. Hapa ni baada ya kunusuriwa na askari

Post a Comment

 
Top