BOIPLUS SPORTS BLOG

London, Uingereza
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford amechaguliwa katika kikosi cha wachezaji 23 watakao wakilisha taifa hilo katika michuano ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao.

Nahodha Wayne Rooney ataendelea kuwaongoza 'Three Lions' sambamba na Harry Kane, Jamie Vardy, Daniel Sturidge na chipukizi huyo kutengeneza safu ya  ushambuliaji.

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu kinda huyo ambaye jana alisaini mkataba mpya na United kuitwa na kocha Roy Hugson baada ya kufunga goli lake la kwanza Ijumaa iliyopita dhidi ya Australia na kuonesha uwezo mkubwa uliomfanya kuwa chaguo la kwanza katika ushambuliaji kwa klabu yake ya Mashetani Wekundu.

Kikosi kamili cha Uingereza
Makipa ; Joe Hart( Manchester City), Freiser Foster ( Southampton), Tom Heaton( Bunley)

Mabeki
Nathan Clyne( Liverpool), Chris Smalling( Man United), Gary Cahill(Chelsea),Kyle Walker( Spurs) Danny Rose( Spurs) John Stones (Everton), Ryay Bertrand (Southampton)

Viungo
James Milner,Adam Lalana, Jordan Henderson( Liverpool), Rahim Sterling ( Man City), Erick Dier, Dele Alli( Spurs) Jack Wilshere( Arsenal), Ross Barkley ( Everton)

Washambuliaji
Wayne Rooney, Marcos Rashford (Man united) Harry Kane(Spurs) Jamie Vardy( Leicester City) Danny Sturridge ( Liverpool)

Post a Comment

 
Top