BOIPLUS SPORTS BLOG

MILAN, Italia
REAL Madrid imefanikiwa kunyakua ubingwa 11 wa klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuifunga Atletico Madrid kwa mikwaju ya penati 5-3 katika uwanja wa San Siro.

Mchezo huo ulilazimika kwenda katika muda wa nyongeza baada ya miamba hiyo kutoka nchini Hispania kutoka sare ya goli 1-1 katika dakika 90 za kawaida.

Real ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Sergio Ramos dakika ya tisa baada ya kumalizia mpira wa faulo uliopigwa na Tony Kroos na kuendelea kulisakama lango la Atletico.

Mshambuliaji Antonio Griezmann alikosa mkwaju wa penati dakika ya 48 baada ya Fernando Torres kufanyiwa madhambi na Pepe katika eneo la hatari. Alikuwa Ni Yannick Ferreira Carrasco aliyewasawazishia vijana wa Diego Simeone baada ya kufunga goli safi dakika 79.

Baada ya kutoka sare na kwenda katika muda wa nyongeza ndipo ilipoamuliwa mikwaju ya penati na waliopata kwa upande wa Real ni Lucas Vasquez, Marcelo, Bale, Ramos na Cristiano Ronaldo aliyefunga ya ushindi.

Atletico waliofunga ni  Griezman, Saul Niguel, Gabi na aliyekosa ni Juanfran.

Mwaka 2014 timu hizo zilikutana fainali kama hiyo na Real kushinda kwa magoli 4-1.

Post a Comment

 
Top