BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Nitike Ahazi, Dar
KIUNGO wa Mbeya City, Ramadhan Chombo 'Redondo' amesema kazi yao ni kupambana uwanjani na kuhakikisha timu inafanya vizuri lakini msimu ukimalizika watawaachia viongozi wafanye kazi yao huku akiweka wazi kwamba Mbeya City ingeshuka daraja ni aibu kwao wakongwe.

Redondo aliiambia BOIPLUS kuwa: ''Ni aibu kuwepo wachezaji kama sisi halafu timu ishuke daraja, tunapambana kadri tuwezavyo ili kuiweka mahala pazuri na kubaki  kwenye ligi hapo tutakuwa tumekamilisha majukumu yetu," alisema.

Redondo alisema kuwa Mbeya City imekuwa ikifanya vibaya kutokana na  uchanga wa wachezaji ambao wamepandishwa kutoka kikosi chao cha timu ya vijana, hivyo hawana uzoefu mkubwa.

"Vita ipo kwetu ambao tunafanya kazi ya kuzinasua timu na hatari ya kushuka na wenzetu wanasheherekea ubingwa hapo ndipo unaona maisha yametofautiana," alisema Redondo.

Post a Comment

 
Top