BOIPLUS SPORTS BLOG

✏GENK, Ubelgiji
TIMU ya KRC Genk imefuzu kushiriki michuano ya Europa baada ya kuifunga Charleroi magoli 5-1 katika mechi ya mzunguko wa pili iliyofanyika  uwanja wa Cristal Arena.

Genk itaanza katika hatua ya mtoano kabla ya kuingia katika makundi na endapo itapita itakutana na miamba ya soka barani Ulaya kama Manchester united, Liverpool na nyinginezo.

Katika mchezo wa awali Genk anayochezea nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ililala kwa magoli 2-0 katika uwanja wa Stade du Pays de Charleroi.

Ili kufuzu katika hatua hiyo Genk ilitakiwa kushinda magoli 3-0 lakini katika mchezo wa leo miamba hiyo ya Ubelgiji ikafanikiwa kufanya kufuru.

Magoli ya Genk yalifungwa na Nikos Karelis aliyefunga matatu 'hattrick' dakika 20, 56 na 71 huku mengine yakifungwa na Samatta 27 pamoja na Sand Walsh.

Mchezo huo ulisababisha nahodha huyo wa Stars kushindwa kuhudhuria katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na kutoka sare ya goli 1-1 jioni ya leo.

Post a Comment

 
Top