BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KIUNGO wa zamani wa timu ya Manchester United Paul Scholes amefunguka kuwa kocha Jose Mourinho atarudisha heshima ya klabu hiyo iliyopotea tangu alipostaafu Sir Alex Ferguson.

Scholes alisema Mreno huyo atajifunza kutoka kwa uzoefu wa Louis van Gaal na kuimarisha kikosi cha mashetani Wekundu  iwapo atachaguliwa kuwa mkufunzi wa timu hiyo.

Mazungumzo ya United na Mourinho yameingia katika siku yake ya pili na kuna kila dalili ya kocha huyo kupewa kibarua cha kukinoa kikosi hicho.

Van Gaal alifutwa kazi siku ya Jumatatu ,siku mbili tu baada ya kushinda kombe la FA.

''Mashabiki katika klabu ya Man United wanahitaji mchezo wa kufurahisha na nina hakika Mourinho atafanikisha hilo," alisema Scholes.

Van Gaal aliiongoza United hadi nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza lakini alikosolewa kwa mchezo wake usio na mashambulizi huku timu hiyo ikifunga mabao 49 tu msimu huu.

Post a Comment

 
Top