BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajiwa kutua leo  saa 1.15 usiku baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini India (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Serengeti Boys haikuwahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano hiyo baada ya kutoka sare mechi tatu na kushinda mmoja kabla ya kuingia hatua ya kucheza mshindi wa tatu ambako ilishinda mabao 3-0 jana dhidi ya Malaysia.

India iliandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwakani.

Post a Comment

 
Top